Semina Ya Uwekezaji na usimamizi wa fedha

1. Walengwa
Semina hii imelenga wafanyabiashara na wafanyakazi ambao ni wateja wa
EFL na wasio wateja katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na
Dodoma. Semina imekusudia kuwaleta pamoja washiriki wenye uhitaji wa
kujenga miradi ya uwekezaji na biashara zao kwa kuwekeza sehemu sahihi
na kulinda fedha zao zisipotee. Imewalenga pia wafanyakazi wanaojiandaa
kustaafu kutoka katika ajira zao kwa miaka yakaribuni.

2. Mada zitakazofundishwa
Mada kuu zitakazofundishwa zitakuwa kama ifuatavyo:
1. Uwekezaji katika Miradi ya kibiashara na kuisimamia
2. Uwekezaji katika Masoko ya Fedha
3. Kuwekeza katika vyanzo vya kipato tulivu (passive income)
4. Kusimamia Mikopo na kuzalisha
5. Bima kwa manufaa ya wafanyabiashara na wafanyakazi.

3. Wawezeshaji wa semina
Mafunzo yatawezeshwa na Professor Goodluck Urassa (UDSM), Mr.Clement
Z .Kwayu Mkurugenzi wa Bumaco Insurance Co.ltd na Wafanyabiashara
mashuhuri watakaokuja kutoa uzoefu wao.

4. Utaratibu utakotumika kuendesha semina
Semina hii itaendeshwa kwa njia shirikishi ambapo washiriki watapata
nafasi ya kushirikishana uzoefu, kushiriki katika mijadala mbalimbali na
kuuliza maswali. Washiriki wataruhusiwa kuleta bidhaa zao, vipeperushi na
taarifa nyingine za biashara zao kuzitangaza. Wataalamu wa UTT na bima
watakuwepo kwa ajili ya kutoa uzoefu wa uwekezaji na bima, na kujibu
maswali ya washiriki. Kwa watakaopenda kuwekeza watapata ushauri na
usaidizi ili waweze kuwekeza. Semina hii Inatarajiwa itawawezesha
washiriki kujenga mtandao wa kibiashara pia kwa ajili ya kujifunza zaidi.

5. Kuhusu gharama
Semina hii imefadhiliwa na EFL na wabia wake kama sehemu ya huduma
za Kijamii. Hivyo, hakuna gharama yeyote ya kushiriki.

JISAJILI: +255 758 978 736 / +255 677 226 960


Hits (276)

copyrights © 2024 123Tanzania.com   All rights reserved. Designed & Maintained by Powerweb